Kutokana na kuongezeka kwa bei za mafuta ya gari na kupanda kwa hali ya maisha, watu wengi wameshindwa kuimili gharama za magari yao.
Ndio maana sasa inakuwa ni kitu cha muhimu kwa wamiliki wa magari kufikiria namna tofauti za kupunguza matumizi katika magari yao na hivyo kuokoa fedha kwajili ya mahitaji mengine ya kifamilia au binafsi.
Baadhi ya njia sahihi za kupunguza gharama za mafuta ni;

1. Panga safari zako ili kupunguza kilometa unazotembea

Panga safari zako zote na uziunganishe pamoja. Kama unaenda kazini kila siku na unahitaji kupeleka watoto shuleni,basi panga hizo zifanyike katika safari moja badala ya kila moja peke yake. Fikiria kutembea badala ya kuendesha gari kwa safari za karibu. Ni nzuri kwa afya pia.

2. Pasha Moto Gari lako kwa muda mfupi tu
Huhitaji kupasha moto gari lako kwa muda mrefu unapowasha asubuhi kama wengi wanavyofikiri na kufanya. Magari ya kisasa yanahitaji sekunde 30 tu za kupshwa moto. Kuacha ingini iwake bila kazi kwa dakika kadhaa tu unapoteza mafuta mengi bila sababu na kuchafua mazingira kwa kutoa gesi ya ukaa.

3. Jaza mafuta mapema asubuhi au jioni
Nunua mafuta wakati wa asubuhi au jioni. Mafuta yanakuwa mazito zaidi wakati huu ambapo joto liko chini. Hivyo unapata mafuta mengi zaidi kuliko wakati wa mchana.

4. Endesha na Ongeza Mwendo Taratibu.
Kuendesha gari kwa kasi kunaweza kukawa kunatia raha lakini kunatia hasara mfukoni mwako. Kuendesha gari kwa kasi ndogo na kuongeza mwendo taratibu(kukanyaga mafuta taratibu) kunatumia mafuta vizuri.

5. Kufuatilia Wakati na jinsi Kupiga Breki

Kufunga breki kwa haraka kunakula mafuta kwa wingi na pia kunamaliza breki zako.Acha umbali wa kutosha katiyako na gari la mbele unapokuwa kwenye foleni za magari. Hilo litakusaidia kupunguza mwendo taratibu.

6. Kuzima injini
Zima injini kila mara unaposubiri mtu. Usiache gari likiwaka bila kazi. Mafuta mengi yanatumika injini inapozunguka gari likiwa limesimama. Lakini pia moshi unaotoka ukiwa umesimama unasababisha uchafuzi mkubwa wa hewa.

7. Unapokuwa barabara kuu na katika mwendokasi wa juu funga madirisha au dirisha la juu

Unapoikimbiza gari kwa mwendo kasi wa zaidi ya 80kph hususani kwa umbali mrefu bila kupunguza mwendo…muundo wa gari lako unamata sana,,,kwanini kwa sababu watengenezaji wa gari hilo waliliunda kwa namna ambayo litaweza kukabiliana na upepo hivyo kurahisisha uendaji wake, sasa ukiweka madirisha wazi wakati wa mwendo mkubwa unaruhusu hewa ndani ya gari na matokeo yake ni kuathiri mwendokasi wa gari lako na hatimae kuathiri namna gari linavyotumia mafuta.

8. Epuka vituo vya mafuta karibu na barabara kuu

Kituo cha kwanza mafuta ambayo utakutana nacho barabara kuu ni wazi kitakuwa na bei za juu za mafuta. Angalia vituo vya mafuta katikati ya mji ili kupata mafuta kwa bei nafuu.
9. Angalia Upepo wa Matairi Yako
Kuendesha gari ukiwa na matairi yenye upepo kidogo husababisha kuisha kwa haraka na kuongezeka kwa matumizi ya mafuta. Matairi yenye upepo wa kutosha hupunguza msuguano na barabara hivyo kusababisha matumizi mazuri ya mafuta.

10. Rekebisha Injini Mara kwa Mara

Injini ya gari inahitaji kuangalia na kufanyiwa marekebisho mara kwa mara. Injini inayopata huduma hutumia mafuta vizuri. Badilisha oili ya enjini kila mara unapopeleka gali kufaniwa matengenezo(“Service”) .

11. Mabadiliko ya Chujio

Angalia chujio za mafuta (“Fuel Filter”) na hewa (“Air filter”) mara kwa mara – hasa kama unaishi au kusafiri maeneo yenye vumbi. Chujio safi zinasababisha gari kwenda kasi zaidi na kutumia mafuta vizuri.

12. Matumizi sahihi Oil

Tumia oili sahihi na safi kwenye gari lako. Angalia kitabu cha muongowa gari lako kama huna uhakika.

13. Punguza matumizi ya kiyoyozi

Kuna kasumba hususani miji au maeneo yenye joto madereva kutumia kiyoyozi kila wakati bila kujali ni majira gani,iwe wakati wa joto,baridi,unyevu nk yeye na kiyoyozi tu…Aah ndugu yangu unameza mafuta bila sababu, be conscious na pesa zako (hata kama zipo tele) nidhamu ya matumizi ni utamaduni mzuri, hata kama husave kwa ajili yako save for the needy au kwa ajili ya mazingira.

Kama eneo ulilopo halina vumbi na hali ya hewa si ya joto sana inapobidi shusha vioo vya gari lako tumia hewa asili , kula upepo kwa raha zako, aircon wakati wote pia inaweza kuwa si salama kwa afya yako, mind you ile ni artificial air.
14.Chagua Njia nzuri

Kila inapowezekana, chagua njia fupi na yenye vizuizi vichache vya barabarani. Njia yaenye foleni ndefu itasababisha matumizi makubwa ya mafuta.

15. Nunua au Endesha Gari Lenye Kutumia Mafuta Kidogo

Kufikiria kununua na kuendesha gari lenye matumizi mazuri ya mafuta. Kwa miji ambayo ina foleni ndefu kama Dar es Salaam,Tanzania au Kampala, Uganda magari madogo chini ya cc 1000 ni chagua bora zaidi. Baadhi ya magari ya aina hii yana uwezo wa kwenda hadi kilometa 40 kwa lita moja ya mafuta.
Image result for car fueling

click HERE to go to listing pages.
click HERE to go to mitandaoni pages.

Leave a Reply