Ofisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Joyce Amon amefikishwa katikaMahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtakala kushawishi rushwa.
Decemba 12,2017 katika eneo la Gerezani Kariakoo Wilaya yaIlala mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa TRA kama Ofisa Msaidizi wa Kodi alishawishi rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiwezekumwandikia cheti cha faini cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Katika shtaka la pili, mwanafunzi Lilian Wilson (23) naye anakabiliwa na shtaka la kusaidia kutenda
kosa hilo.
Wakili Nyanda amedai Desemba 13,2017 katikaHoteli ya Tansome mshtakiwa huyo Lilian alimsaidia Joyce ambaye ni Ofisa Msaidizi wa Kodi waTRA kujipatia Sh400,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiweze kumpatia cheti cha faini cha VAT.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa
upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Sachore alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka katika taasisi zinazotambulika kisheria ambao watasaini ahadi ya Sh5 milioni kwa kila mmoja. Na kwamba barua hizo zitahakikiwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20, 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi
utakuwa umekamilika au la.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply