Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alifananisha klabu yake na bondia ambaye anajikakamua kuinuka baada ya kupigwa kondena kuangushwa ulingoni na jinsi klabu hiyo ilivyojikwamua na kulaza AC Milan 2-0 katika Europa League baada ya msururu wa matokeo mabaya.

Wenger alisema pia kwamba matatizo hayadumu.
Image result for arsenal wenger

Arsenal walikuwa wanakabiliwa na uwezekano wa kushindwa mara ya tano mtawalia wka mara ya kwanza tangu 1977 walipoandikisha ushindi huo wa kuvutia uwanjani San Siro.

Mabao kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan – aliyetawazwa mchezaji bora wa mechi – na Aaron Ramsey yaliwaweka vijana hao wa Wenger katika nafasi nzuri ya kufika robo fainali katika ligi hiyo ndogo ya klabu Ulaya.

“Ni ushindi muhimu sana kwa sababu tulikuwa na wiki ya masaibu,” alisema Wenger.

Gunners walikuwa wamecharazwa na Brighton katika Ligi ya Premia Jumapili, baada ya kulazwa mara mbili mfululizo 3-0 na Manchester City katika fainali ya Kombe la Ligi uwanjani Wembley na katika Ligi ya Premia.

Aidha, walikuwa wamelazwa pia 2-1 na wanyonge wa Sweden Ostersunds FK, ambapo walinusurika kutokana na ushindi wao mkubwa mechi ya kwanza na kusonga hadi hatua ya 16 bora ambapo walipangwa kucheza na Milan.

click HERE to go to listing pages.
click HERE to go to mitandaoni pages.

Leave a Reply