Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town – mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji – kuwa janga la kitaifa.

Serikali ilitoa tangazo hilo baada ya kukagua upya ukubwa na athari ya ukame huop wa miaka mitatu. Umeathiri vibaya majimbo matatu ya majimbo tisa nchini humo.

Uamuzi huo umejiri wakati Cape Town umetangaza kuwa hatua za kupunguza matumizi ya maji, zinazohitaji kila raia asitumie zaidi ya lita 50 za maji kwa siku – imesaidia kuisogeza mbele “Day Zero” siku ambayo mji utakuwa hauna hata tone la maji hadi Juni 4.
Miji 11 iliyo kwenye hatari ya kukumbwa na ukosefu wa maji ya kunywa kama Cape Town, Ni wiki chache tu zilizopita tarehe iliyotolewa wakati mabomba yalitarajiwa kukauka Cape Town ilikuwa ni Aprili 12.

Mmusi Maimane, kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA), kinachosimamia miji ya Cape Town na jimbo la Western Cape province, alisema katika ujumbe wake wa Twitter:

Kiwango cha maji yanayotumika kwa wastani katika mji wa Cape Town, mji ulio na takriban watu milioni 4, ni chini ya lita milioni 550. Miaka miwili iliyopita ilikuwa ni zaidi ya lita bilioni kwa siku.

…………………………………………………………………………………………………………………..
Unaruhusiwa kuweka matangazo yanayohusu 1.kuuza/kukodisha gari, 2.kuuza/kukodisha nyumba, 3.Kuuza /kukodisha kiwanja, 4.kuuza / kukodisha nguo, 5.kuuza vifaa vya electronics kama Simu, Computer, na matangazo mengine
Karibu mitandaoni classfied website —-online market….

Leave a Reply