Mkuu wa Mkoa DSM Makonda, anasema Pasaka hii hakuna Waraka toka jiji la Dar. Watu wameabudu kwa amani kabisa. Pia amezungumzia watu kutoka mikoa mingine na kuja kutoa kauli za uchochezi Dar na kusema wanajipanga kudhibiti hilo maana Dar ni Jiji la kibiashara linalohitaji utulivu.

Rais Magufuli: Hivi sasa tunapoteza tozo la Bilioni 1 kutokana na sehemu ya anga letu kukasimiwa kwa Kenya. Nina imani mradi ukiisha wataturudishia.

Rais Magufuli: Nchi hii uwezo wake ni mkubwa mno. Ndio maana watu wengine wenye wivu wanaumia sana. Wenye wivu wapo, hata Mungu aliumba malaika wakaja wenye wivu Mashetani wakatupwa huku duniani.

Tukanunua ndege 6 bila kukopa. Zilipokuja hao hao waliokuwa wanaponda ndio wa kwanza kupanda hizo ndege. Tunawasamehe sana

Ninafahamu hata makanisani zaka zimepungua sababu zilikuwa zinatolewa na mafisadi.

Ilifikia kipindi hata kwenda Kibiti ilikuwa shida, hatukuona mtu analaani. Hakukuwa na Waraka wala nini. Sipendi kuzungumzia hili maana halina maana. Wengine nawacheki tu nasema ” Hiiiiiiiiii”

Baba wa Taifa alishasaidia nchi nyingine kupata uhuru. Jukumu langu mimi sasa ni kujenga uchumi wetu!
Katika juhudi hizi watatokea wa kunung’unika, wa kupiga kelele hata sitawasikiliza.

Kazi ya uongozi ni ngumu sana, unageuka huku unakuta watu wanalalamika. Hata Wakina Musa walipata shida, unawavusha watu unakuta wengine wameshajenga na sanamu la dhahabu.

Serikali ipo haijalala na haitalala. Usimuone Simba amelala ukamchezea Mkia.

>>> Nafasi mbali mbali za kazi
>>> Simu inauzwa: Samsung A5
>>> Weka Tangazo lako Hapa
>>> Fungua hapa kwenda ukurasa wa Mbele

Leave a Reply